Visit Sponsor

Written by 3:04 pm KITAIFA Views: 46

RAIS SAMIA ATEUA MAJAJI WAPYA SITA MAHAKAMA YA RUFANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameteua Majaji sita wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi Zuhura Yunus leo tarehe 18 Mei, 2023 imesema uteuzi huo umeanza tangu tarehe 28 Aprili, 2023 na wateule hao wataapishwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Walioteuliwa ni Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Zainab Goronya Mruke na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania, Mhe. Dkt. Benhajj Shabaan Masoud.

Taarifa hiyo inawataja wateule wengine ni aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora ambaye kwa sasa anahudumu katika Kanda ya Shinyanga kwa nafasi hiyo, Mhe. Amour Said Khamis na Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es Salaam, Mhe. Leila Edith Mgonya.

Wengine ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson John Mdemu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Agnes Zephania Mgeyekwa.

Uteuzi huo unaongeza idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani kutoka 26 waliopo hivi sasa hadi 32.

About The Author

(Visited 46 times, 1 visits today)

Last modified: May 30, 2023

Close