Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
-DAR ES SALAAM
NI kampeni za lala salama. Ndivyo unaweza kusema, hasa baada ya vyama vya siasa nchini kupepetana kwa siku saba kwenye majukwaa ya kisiasa kusaka ushawishi kwa wananchi.
Kutokana na hali hiyo sasa Watanzania leo wataamua kwa kupiga kura ili kuchagua wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji huku CCM ikitamba kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo.
Kutokana na hali hiyo timu wa wabunge na madiwani wote wa CCM sasa imepiga kambi kwenye majimbo ili kusaka kura ambapo Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa jimbo la Ubungo, alisema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo sababu ya wananchi kuchagua Chama Cha Mapinduzi.
Rais Samia atoa rai Kwa wananchi kushiriki uchaguzi huu kwa amani na upendo huku akihusia vijana kuacha kujichanganya na mambo maovu hasa chuki na matukio yasiyokuwa ya kiungwana kuelekea uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
About The Author
Last modified: December 3, 2024