Visit Sponsor

Written by 1:27 pm KITAIFA Views: 56

PRUDENCIA PAUL KIMITI (MBE) RASMI BODI YA UTALII TANZANIA

Huyu ni Mtanzania ambaye ni mkuu wa kitengo cha forodha katika idara ya Huduma za upelelezi wa tuhuma za udanganyifu katika kulipa kodi ya Taasisi ya mapato nchini Uingereza, na anaushawishi mkubwa nchini humo, lakini pia akitumia muda wake mwingi kama mwanaharakati wa haki za watu weusi, alitambuliwa na kupewa tuzo ya heshima kubwa na Malkia Elizabeth II enzi za uhai wake. Leo Tarehe 11 Januari 2024 ametembelea Bodi ya Utalii Tanzania na kueleza dhima yake ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza na kuupeleka utalii wa Tanzania katika viwango vya juu zaidi, akiongea na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Masoko TTB Dkt. Gladstone Mlay amesema “tumefurahishwa na ziara hii adhimu na tumemkabidhi zana za kutangaza utalii na kupanga mkakati wa kuhakikisha tunaitangaza zaidi Tanzania kupitia mtu huyu mashuhuri Duniani.

About The Author

(Visited 56 times, 1 visits today)

Last modified: January 11, 2024

Close