Na Dr. Bravious Kahyoza
Wakati zoezi la mafunzo na kuibua miradi kwa awamu ya pili kwenye halmashauri zote nchini likiwa wiki ya tatu sasa, mkoani Katavi zoezi hilo limeendelea kwenye halmashauri za wilaya ya Tanganyika na Nsimbo.
Zoezi hilo linaloratibiwa na Kituo cha Ubia(PPPC) limeendelea kuwa na mvuto wa aina yake likiwa na mijadala fikirishi, maoni na ushauri kutoka kwa wataalam wa halmashauri husika.
Dkt Bravious Kahyoza anayeratibu zoezi hilo mkoani hapa, analitaja kama zoezi lililoamsha ari ya ubia kwa viongozi na watendaji wa halmashauri hizo. Naye Michael Kihanga, mratibu mwenza wa zoezi hilo, analiona kama hatua ya mwamko mpya wa shughuli za ubia kwenye uendeshaji wa uchumi wa serikali za mitaa nchini.
Wakati wa zoezi hilo kwenye halmashauri za Tanganyika na Nsimbo, masuala muhimu yaliyozingatiwa kama maelekezo ya Kituo cha Ubia ni pamoja na kuelewa dhana ya PPP na kuibua miradi yenye sifa ya utekelezwaji wa ubia, kuandaa maandiko dhana (Project Concept Notes), kuandaa matangazo ya miradi kwa wawekezaji pamoja na kutumia teknolojia ya GIS katika uwekaji wa miradi kwenye ramani za Halmashauri.
Idadi ya wataalamu waliopatiwa mafunzo
Michael Kihanga anasema kuwa jumla ya wataalam 39 kwenye halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika walipatiwa mafunzo na wataalam 12 katika halmashauri ya Nsimbo walinufaika na mafunzo hayo.
Idadi hii ya wataalam waliopata mafunzo haya inalenga kujibu kiu ya PPPC ya kuwafikia watendaji wengi wa serikali wenye uelewa wa dhana ya PPP.
Akieleza azma hiyo wakati wa kuandaa timu ya wataalam kutoka PPPC na Vyuo Vikuu kwenda mikoa yote nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo, mkuu wa idara ya uendelezaji miradi, Bw. Innocent Mauki alisisitiza alikuwa na haya ya kusema;
“Tunatamani kuona miradi ya maendeleo yenye mvuto wa kutekelezwa na sekta binafsi ikiandaliwa kwa utaratibu wa PPP ili kufikia azma ya kuweka PPPs kwenye kitovu cha menejimenti ya uchumi wa halmashauri zetu. Hata hivyo, hili litategemea sana na jinsi PPPC itakavyofikisha uelewa wa dhana hii kwa wataalam hao. Na hilo ndilo jukumu mnalokwenda kulifanya”
Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika inazo fursa mahbuba nyingi zenye kuweza kuwa na mvuto wa PPP kuanzia kwenye shughuli za utalii, usafirishaji, kilimo, ufugaji na masoko ya biashara.
Wakati akitoa mafunzo hayo, Dkt Kahyoza ametaja faida za kuendesha miradi kwa mfumo wa PPP kuwa ni pamoja na kusaidia katika rasilimali fedha, kufanya miradi kwa ubunifu na ujuzi mkubwa na ufanisi wa kiwango cha juu katika utoaji wa huduma.
Wakati wa mjadala na watendaji wa halmashauri ya Tanganyika baada ya mafunzo, mkuu wa wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu aliahidi ushirikiano kwa PPPC na kushauri kituo kuzitazama fursa zinazoweza kuwakwamua wananchi wengi kutoka kwenye umskini.
“Tunafurahi kuwa PPPC mmetufikia hapa Tanganyika, ni maoni yangu kuwa muweke nguvu kwenye miradi inayoweza kuwakwamua wananchi kwenye umaskini kama kilimo na ufugaji. Kwa mfano hapa Tanganyika, PPPs zinaweza kuwa na msaada mkubwa kwenye masoko ya mazao, minada ya kuuzia mifugo na miundombinu”. Alisema Mhe. Onesmo
Mhe. Buswelu aliongeza kuwa, miradi ya soko la kimataifa na sehemu ya kisasa ya maegesho ya malori inaweza kuwa miradi maridhawa ya ubia kwenye ukanda wa bandari ya Karema.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Dkt. Alex Mrema, alisisitiza juu ya fursa za PPPs kwenye ukanda wa bandari ya Karema. Dkt. Mrema aliitaja bandari hiyo kuwa ya muhimu sana kwa uchumi wa nchi kwani kwenye ukanda huo kuna fursa nyingi zinazotakana na biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Halmashauri ya Nsimbo
Halmashauri ya Nsimbo iliyo karibu na Manispaa ya Mpanda inazo fura za ubia kwenye maeneo ya masoko ya mazao, maghala kwa ajili ya mazao ya kilimo na miundombinu ya usafirishaji na biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo, Bi. Christine Bunini, anayapokea mafunzo ya ubia kama chachu ya kusukuma maendeleo ya uchumi wa halmashauri hiyo.
“Hapa Nsimbo tutajitahidi sana kuhakikisha tunapata fursa za ubia kama PPPC inavyohanikiza. Hizi tunaziona kama jitihada za makusudi za kituo katika kuweka kwenye vitendo fikra za Mhe. rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuifanya sekta binafsi kuwa chachu ya uchumi”
Akieleza jinsi dhana ya ubia inavyofanya kazi kwenye mafunzo hayo Dkt. Kahyoza amefafanua kuwa mambo muhimu ya kuzingatia katika miradi ya PPP ni Kuishirikisha Kituo cha Ubia katika maandalizi ya miradi inayohusisha ubia kwa maoni. Aidha, kabla ya kusaini mikataba inayohusisha ubia na Sekta Binafsi, Mamlaka za Serikali inapaswa kujiridhisha kuwa Sheria ya PPP na Kanuni za PPP za mwaka 2020 zimezingatiwa
Akitoa maoni jinsi halmashauri ya Nsimbo inavyoweza kunufaika na PPPs, Afisa Biashara wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni mtaalam wa PPP, alisema Nsimbo ina fursa kwenye uibuaji wa viwanda na hasa viwanda vya mazoa ya kilimo na hata vile vya vinywaji laini kama maji ya kunywa.
Tafakuri ya Kasi ya Ongezeko la Watu, Ukuaji wa Uchumi na PPPs
Kasi ya ongezeko la watu Katavi uko 7.2% na ukuaji wa uchumi 6%
Mkoa ambao una ukuaji wa uchumi (GDP) ya wastani wa 6% juu ya kiwango cha kitaifa cha 5.6%; kwa haraka unaweza kuona unafanya vizuri.
Upande wa pili ni kuwa, hii si hali nzuri ukilinganisha na hali ya kitaifa. Hii maana yake ni kuwa, pato la mtu mmojammoja (per capita income) la Katavi linakua kwa kiwango hasi wakati la kitaifa linakua kwa kiwango chanya. Kwa kasi ya ukuaji wa watu ya 7.2% na ‘ukuaji wa uchumi” wa 6% , maana yake pato la mtu mmoja linakua kwa -1.2%( GDP growth rate -population growth rate).
Wakati huohuo hali ni tofauti kitaifa. Kwa ukuaji wa uchumi wa 5.6% na ukuaji wa idadi ya watu ya 3%, ukuaji wa pato la mtu mmojammoja ni 2.6%.
Kwenye mkoa wenye sura hii ya kiuchumi pamoja na kuwa na rasilimali lukuki, waliotahabaria au wanaotaka kutabaharia kwenye masuala ya PPPs tukiongozwa na PPPC, iko haja ya kuongeza sababu za kwa nini PPPs ni muhimu sasa kuliko jana.
Zifuatazo ni sababu za kwanini PPPs ni muhimu:
1.PPPs ni njia ya kurasimisha shughuli za kiuchumi. Kwa mfano wilaya ya Tanganyika, wafanyabiashara kutoka Sudan Kusini, Somalia, DRC n.k wanawatumia wazawa kuwanunulia mifugo na mazao kwa njia za panya na hivyo kuathiri thamani halisi ya kiuchumi ya sekta ya mifugo ya kilimo. Kama mnada wa mifugo wa Sibwesa wilayani Tanganyika kwa mfano, ukifanyika kwa njia ya ubia, utakuwa wa kisasa na kufanya urasimishaji wa shughuli za mauzo ya mifugo.
Hali kama hii tuliikuta halmashauri ya Mlele ambako Mkurugenzi wa Halmashauri alisema kuna uzalishaji wa mchele na nyama kwa wingi, lakini kuwaona wakulima na wafugaji ni muhali. Sina shaka kuwa, ile sababu ya kurasimisha shughuli za kiuchumi anayotaja hayati rais Benjamin Mkapa kwenye MY LIFE, MY PURPOSE kama sababu iliyomfanya amlete mchumi nguli De Soto awe mshauri wake, bado ni sababu kubwa ya kwa nini tunataka PPPs leo.
- Nafikiri PPPs ni njia ya kuvuna potentials za uhamiaji wa ndani wa kiuchumi kwenye mikoa ya pembezoni kama Katavi. Hapa Katavi kuna wakimbizi wa kiuchumi kutoka mikoa mingine wakijikita kwenye ufugaji na kilimo. Shida kubwa ni kufanya bila urasimishaji, lakini zaidi serikali haina njia yenye ufanisi ya kuendesha uchumi wa sekta hizi kwa manufaa ya wananchi. PPPs inaweza kuwa dawa ya hili.

About The Author
@ppp_centre_Tz #pppcentretanzania
Last modified: April 11, 2025