Visit Sponsor

Written by 3:05 pm KITAIFA Views: 102

POLISI WAONYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime

Hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya vitendo vya kihalifu ambavyo havikubaliki, siyo utamaduni wa watanzania lakini pia ni kinyume cha sheria za nchi

Tumeshuhudia Februari 21, 2024 huko mkoani Manyara, wilaya ya Babati, katika eneo la Magugu, wananchi walifanya vurugu na kufunga barabara wakishinikiza Jeshi la Polisi liwakabidhi mtuhumiwa aliyekuwa akituhumiwa kumbaka kisha kumuua mtoto wa miaka saba.

Pia, Febuari 27, 2024, mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe, eneo la Msambiazi, waendesha bodaboda waliteketeza kwa moto basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya safari zake Dar es Salaam Arusha baada ya basi hilo kumgonga dereva wa bodaboda ambaye alifariki dunia.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa baadhi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi kuacha tabia hiyo ambayo ni kinyume cha sheria n ani ukiukwaji  wa misingi ya haki za binadamu. Kitendo cha kuchoma basi kimedhulimu haki za watu wengine ambao hawakuhusika na tukio hilo la ajali kwani mali za abiria ziliteketea kwa moto na kuwaingiza katika hasara kubwa na pengine kuwarudishwa kwenye umaskini. Pia basi lililochomwa, kimemwingiza mmiliki kwenye hasara ambayo siyo sahihi kwani kilichotakiwa ni kusubiri vyombo vinavyosimamia sheria vichukue hatua dhidi ya dereva kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.

Pia Jeshi la Polisi liatoa wito kwa baadhi ya bodaboda wenye tabia kama hizo wajitafakari, waelimishane na wajiulize je sisi nasi tunafuata sheria za usalama barabarani? Hali kadhalika wajiulize na sisi tunavyo vunja sheria pikipiki zetu zichomwe moto? Niwazi kwamba jibu ni Hapana na si sahihi mbele ya sheria.

Wajitafakari kwa namna hiyo ili waache kujichukulia sheria mkononi ambayo ni kosa kisheria lakini pia hakuna anayependa wala kutamani kufanyiwa kama walivyofanya hao bodaboda wa tukio lililotokea Wilayani Korogwe.

Jeshi la Polisi linaendelea kwa nguvu zote kuwasaka waliofanya uhalifu huo wa kuchoma basi Wilayani Korogwe ili wafikishwe mahakamani.

About The Author

(Visited 102 times, 1 visits today)

Last modified: February 28, 2024

Close