Visit Sponsor

Written by 2:04 pm Uncategorized Views: 29

POLISI LAONYA WATAKAOTOA TAARIFA ZA UONGO WATOTO WA SHULE KUTEKWA

JESHI la polisi limepiga marufuku na kuonya mtu yeyote au kundi lolote linaloeneza taarifa za uongo zinazohusiana na baadhi ya watoto wa shule kutekwa na kuchinjwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime taarifa hizo zimeleta taharuki,mshtuko na usumbufu kwa wazazi na walezi.

“Mbali ya tabia hiyo kuwa kosa la jinai pia unatakiwa ilaaniwe na kukemewa kwa nguvu kubwa na kila mmoja wetu mwenye kuchukia tabia kama hizi za watu wachache”… Alisema DCP Misime.

Aidha Jeshi la polisi limewataka Wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida huku jeshi hilo likiendelea kuwasaka watu hao waaovumisha taarifa hizo za uongo na kisha kuwafikisha mahakamani.

Pia jeshi la polisi limewakumbusha wananchi, wazazi na walezi kuwa wana wajibu wa kuwalinda, kuwasikiliza na kuwatunza watoto.

Pia viongozi wa serikali za mitaaa wametakiwa kusimamia na kuhimiza doria za vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuzuia uhalifu katika mitaa yao.

About The Author

(Visited 29 times, 1 visits today)

Last modified: July 20, 2024

Close