Visit Sponsor

Written by 1:30 pm MICHEZO Views: 22

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAIBUKA NA USHINDI MBIO ZA NYIKA

Watumishi wawili wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora waibuka na ushindi katika mbio za Nyika zilizoandaliwa
kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji
wa shughuli za VVU na Ukimwi hapa nchini.
Katika mbio hizo Bw. Kokolo Lusanda ambaye alishiriki mbio za kilometa
5 aliibuka mshindi wa pili na Bi. Juliana Ntukey aliibuka mshindi wa nne
katika mbio za kilometa 10.


Bw. Kokolo amesema kuwa mashindano hayo ya mbio za nyika
yamemuongezea ari ya kuendelea kufanya mazoezi na kushiriki katika
mashindano mengine yatakayoshirikisha watumishi wa umma kwa kuwa
raha ya ushindi ni kuendelea kushiriki na kushinda katika mashindano
mengine.
Naye Bi. Juliana alibainisha kuwa mbio za nyika zilikuwa na ushindani
mkubwa lakini jitihada zake za kumalizia kama vile ndio anaanza mbio
zimemfanya kuwapita wenzake na kupata nafasi hiyo ya nne kwa
kishindo.


“Nimefarijika sana kuwa mshindi kwa nafasi ya nne sio haba na kwa
mwaka ujao nitaongeza juhudi kubwa ili niweze kushika nafasi ya
kwanza kwa kudra za Mwenyezi Mungu” alisema Bi Juliana.
Aidha, washindi hao wameishukuru Menejimemti ya Ofisi ya Rais-
UTUMISHI kwa kutoa kibali kwa watumishi wake kushiriki kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambapo wametumia fursa hiyo
kushiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, 2023 yanayofanyika Kitaifa
Mkoani Morogoro na kuibuka washindi.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
kupitia Idara ya Uendelezaji Sera ipo mkoani Morogoro kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani
humo ambapo sehemu ya watumishi wake wameshiriki katika mbio hizo
za nyika na kuibuka washindi.

About The Author

(Visited 22 times, 1 visits today)

Last modified: November 28, 2023

Close