
Na Mwandishi wetu Mwanahabari
Dar es Salam
Shirika la bima la taifa NIC INSURANCE yafanya makubaliano ya kufanya biashara na Benki ya Equity kutoa suluhisho la bima za kilimo na mikopo ya kidigitali.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es laam na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima la taifa NIC Insurance Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amesema kuwa wamewekeza katika Benki ya Equity wananchi waweze kukopa ili kukuza na kuendesha shughuli za kiuchumi, lengo ni kuboresha sekta ya kilimo kwa kupata bima na mikopo rafiki.
“ushirikiano huu unaenda kusaidia kuleta faida na kutoa mchango kwa wananchi na kusaidia serikali kuwezesha mafanikio ya kiuchumi kwa wananchi mmojammoja.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Benki Isabela Maganga amesema mteja anaweza kukopa na kupata bima ya maisha, biashara, nyumba na familia kwa ujumla ikiwa imetokea majanga mikopo unaweza kulipwa kupitia bima.
Tumetambua uwezo huo kupitia shirika la bima la taifa NIC na kufanya nao kazi bima la taifa ina uhitaji mkubwa wa masoko hususani kutoka kwa wafanyabiashara wa kilimo.
Aidha Wateja hao tunawafikia kidigatali zaid na tunatoa mikopo kutoka na kukua kwa mikopo yetu asilmia 75 pia mkopo huo unakuwa mtaji kwa mfanyabishara.
Vilevile tunaenda kuendelea kutoa bima kwa wafanyabaishara wote nchini na tunaenda kuhakikisha kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa kilimo na ajali za moto.
Tumeweka Mikakati hii na malengo mahususi ambayo tunaenda kuwafikia wafanyabiashara wengi kupata huduma zetu popote” amesema mkurugenzi maganga
About The Author
Last modified: January 16, 2025