Visit Sponsor

Written by 1:37 pm KITAIFA Views: 5

NAIBU WAZIRI SANGU AGUSWA NA UTU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN  KWA WAVUVI 540 WALIOKOLEWA



Na Mwandishi Wetu – RUKWA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amemshukuru  Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyoguswa na tukio la kuwaokoa Wavuvi 540  waliokuwa wanafanya shughuli za Uvuvi katika Ziwa Rukwa.

Amesema kitendo cha Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan  kutoa helkopta ya Jeshi  iliyoambatana na Wazamiaji wapatao 50 na vifaa maalum vya uokozi inaonesha ni  jinsi gani anavyothamini maisha ya Wananchi wa Jimbo la Kwela na  Mkoa wa Rukwa kiujumla.


Mhe.Sangu ametoa shukrani hizo kwa nyakati tofauti jana  wakati akizungumza na Waumini wa Kigango cha Ilemba na Nankanga mara baada ya misa maalum ya kuwaombea wavuvi hao waliokumbwa na dhoruba ya upepo  mkali  katika ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Amesema vikosi vilivyokuja vilisaidia
kuongeza nguvu za Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi huku akisema vikosi hivyo visingefika kwa haraka wenda athari ingekuwa kubwa zaidi

” Mlimuona  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Innocent Bashungwa,  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji  pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga walifika kuungana nasi ili kuwaokoa ndugu zetu ” amesisitiza  Mhe.Sangu 

Hata hiyo Mhe.Sangu amesema kwa mujibu wa taarifa ya Serikali iliyotolewa hadi kufikia jana ,  jumla wavuvi tisa   kati ya 10 waliokuwa  wanaendelea  kutafutwa tangu  Januari 23, 2025 wamekutwa wamefariki ambapo miili minne ilitambuliwa na ndugu zao  huku miili  mitano imeshazikwa kutokana hali iliyokuwa nayo.


Amewaeleza waumini hao kuwa vikosi vya uokozi bado vinaendelea na kazi ili kumpata mmoja aliyesalia huku akitoa wito kwa wananchi kuleta majina ya ndugu zao ambao hawapatikani tokea tukio hilo lilivyotokea.

Aidha, Mhe.Sangu ametoa pongezi  kwa Wananchi kwa kushiriki kikamkalifu katika uokoaji pamoja na kutoa ushirikiano wa kuwatambua wavuvi wengine ambao walikuwa hawajasajiliwa katika vikundi na makampuni.

Katika hatua nyingine, Mhe.Sangu amewaeleza Waumini hao kuwa Serikali inatarajia kununua boti ya maalum ya kisasa ikayotumika katika ukanda wa Ziwa Rukwa kwa ajili ya shughuli ya uokozi wa  wavuvi pale dhoruba kali ya upepo inapojitokeza.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: January 28, 2025

Close