Visit Sponsor

Written by 1:47 pm KITAIFA Views: 49

NAIBU MEYA KINONDONI AOMBA WATANZANIA KUMSAIDIA MGONJWA KALUME ALLY

Mwandishi: Carren Mgonja

Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni Michael Urio Leo amemtembelea mgonjwa Kalume Ally (41) na kuomba serikali, viongozi wa serikali kujitokeza kwa wingi kumsadia matibabu na huduma za kibinadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumuona Urio alisema Kalume yupo kwenye maumivu makali na kuuomba uongozi wa hospitali kumsadia kwa hali na Mali.

“Nimefika wodini, nimebahatika kumuona ndugu yetu, kwa kweli yupo kwenye maumivu makali sana, ameniambia na nimemuona, ombi langu kwa uongozi wa hospitali ya Muhimbili tumsaidie ndugu yetu huku sisi tukiendelea kuiomba jamiii imsaidie kwa Hali na Mali, naaamini tutafanikiwa” alisema Urio.

Alisema kuwa anaomba mawaziri, wabunge, madiwani na watu mbalimbali kumchagia.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dk Rachel Mhavile alisema, mgonjwa huyo alipokelewa Agost 24 akitokea hospital ya Temeke na tayari ameshafanyiwa vipimo vyote.

“Tayari ameshachukuliwa vipimo vyote na tunangoja vipimo tuone tunaanzia wapi, kwa Sasa anapewa dawa za kutuliza maumivu , ” alisema Dk Mhavile kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Dk Mohammed Janabi.

Mara baada ya mazungumzo na waandishi wa habari Meya Urio alionekana akifuta machozi, kuonyesha kuumizwa kwake juu ya mgonjwa huo, na kuahidi yeye na familia kuchangia waichonacho hivi karibuni.

About The Author

(Visited 49 times, 1 visits today)

Last modified: August 28, 2024

Close