Visit Sponsor

Written by 10:43 am Uncategorized Views: 2

MSIGWA AWAASA WATANZANIA KUJIVUNIA MRADI WA JULIUS NYERERE

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa rai kwa Watanzania kujivunia mradi wa Julius Nyerere kutokana na ukubwa wake si katika bara la Afrika peke yake na Dunia kwa ujumla na kuipongeza Wizara ya Nishati kwa usimamizi wa mradi huo wa kimkakati utakaozalisha Megawati 2115, hivyo kuleta ziada ya upatikanaji wa Umeme nchini.

Msigwa ametoa pongezi hizo leo Februari 16, 2025 katika eneo la mradi wa Julius Nyerere wakati wa Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari wenye lengo la kuzungumzia mafanikio kwenye sekta ya nishati sambamba na maendeleo ya mradi wa kufua Umeme wa JNHPP.

“Wizara hii kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Mhe. Dkt Doto Biteko,inafanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi huu na mingine ambayo inawanufaisha watanzania kwa kuwapatia umeme wa kutosha.” Amesema Msigwa.

Amesema mradi wa bwawa la Julius Nyerere unahusisha mambo makubwa matatu ambayo ni upatikanaji wa umeme, kilimo kwenye umwagiliaji pamoja na uvuvi kwenye ufugaji na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa maslahi mapana ya nchi.

Aidha mradi huo ambao ulianza kujengwa mwaka 2019 kwa gharama ya shilingi trillioni 6.558, hadi sasa umefikia asilimia 99.8 na mashine nane Kati ya Tisa zimesha kamilika ambazo zimeingiza kwenye gridi ya Taifa megawati kwa jumla ya megawati 1,880.

Msigwa amesisitiza kuwa mashine ya mwisho namba tisa utekelezaji wake umefika asilimia 98 huku majaribio ya mtambo huo yakitarajiwa kuanza Februari 25 na Machi 10 utaingiza umeme kwenye gridi ya Taifa ili kukamilisha megawati 2,115.

About The Author

(Visited 2 times, 1 visits today)

Last modified: February 17, 2025

Close