Visit Sponsor

Written by 5:26 pm KITAIFA โ€ข Views: 5

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI SAAD APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI MCHANGA MTO MBEZI

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

Kwa kuelekea kwa Mvua nyingi kunyesha Wilaya ya kinondoni imekuwa ni wahanga wa miundombinu ya Mvua kinondoni inamito Zaidi ya Tisa na kupelekeaย  Mito hiyo kujaa maji pindi Mvua zinaponyesha Mito hiyo Kwa kupanuka na watu kuchimba michanga Katika Kingo za Mito hiyo na kupelekea kuleta changamoto ya mmomonyoko wa Ardhi na kuleta Maafa ya Nyumba kuporomoka na kuharibu mazingira



Kwa Mwaka 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni inaendelea kusimamia mazingira vizuri Ili mazingira yaendelee kuwa salama Kwa Afya zetu pia Kwa uchumi na maendeleo Kwa ujumla inaitaji kuzuia na kudhibiti Kwa kuathirika Kwa watu pindi Mvua zinaponyesha Kwa kukosa makazi Kwa kulala nje na kuharibika Kwa miundombinu ya nchi

Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Saad Mtambule amewataka vijana wanaochimba mchanga Katika Kingo za Mito kuacha mara Moja

Amesema Mto mbezi ni Mto ambao Mvua ikinyesha,na kutokana na udongo wa Mto huo huwa unatanuka,na unapotanuka unasababisha nyumba nyingi na miundombinu mingine ya serikali na watu binafsi inaharibiwa vibaya sana,



“Tunapita Katika hiyo mitaa ikiwa ni sehemu ya Kuendelea kufanya Tathimini ya jitihada na mikakati mbalimbali ambayo tunayoendelea nayo,tumefanya triming ya Mto ya kina na Kingo na kutengeneza tuta pembeni Ili Mvua zitakaponyesha Kuta zisiendelee kubomoka Zaidi pia tumejifunza Kuna kazi gani au Kuna eneo Gani ambalo tunaitaji kulifanyia jitihada Zaidi na haya ni maandalizi ya kuelekea Mvua hizi za mwaka huu wa 2025 na tunaendelea Kwa kushirikiana na wadau Kwa kuhakikisha tunachukua jitihada za kuzingika Zaidi hizo Kingo kuhakikisha kwamba nyumba na maisha ya watu hayaathiriki kutokana na Mvua hizi”.Amesema Mtambule



Aidha Ametoa wito Kwa wakandarasi ambao wamepewa maelekezo na timu maarum iliyoundwa kuhakikisha wanazingatia Yale maelekezo ya usawazishaji ya hiyo Mito wasiende kusawazisha Katika maeneo ambayo hawajaruhusiwa au wasifanye kitu tofauti eti Kwa sababu itakuwa ni kinyume na tutahatarisha mazingira hayo na maisha ya watu.

Pia Amefafanua kuwa makampuni na vijana ambao wanaochimba mchanga tunafahamu vijana Wetu hii ni sehemu ya ajira ila inabidi kufata utaratibu na utaalamu ambao wamekuwa wanatuelekeza mara Kwa mara



“Kama mchanga eneo hili halipo basi ni vizuri kutumia fursa nyingine ambazo zipo kwenye maeneo yetu haya”Ameongeza Mtambule

Pia Amefafanua kuwa Rais Samia ameendelea kuifungua nchi na ameendelea kuhakikisha mifumo na fursa mbalimbali zinakuwepo



“Tuna Zaidi ya billion 9 Katika manispaa ya kinondoni ambayo mie najivunia sana timu ya madiwani na timu ya wataalumu na ikiongozwa na wakurugenzi Kwa kukusanya na kutenga pesa Kwa ajili ya vikundi vya wanawake,vijana na walemavu,vijana pia watumie fursa hizi wa uwepo wa mikopo wa asilimia 10″Amefafanua

Mtambule amefanya ziara kwenye maeneo ambayo hatarishi Kwa Mvua pindi zinaponyesha ametembelea Mto Mbezi (Kwa mboma),Tegeta (msufini),Nyakasangwe (Boko Kwa Mpemba)

About The Author

(Visited 5 times, 2 visits today)

Last modified: January 8, 2025

Close