Visit Sponsor

Written by 11:01 am BURUDANI Views: 128

MIAKA 45 YA SIKINDE, KUANZISHA ACADEMY KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAMUZIKI WAPYA

Kuelekea kuadhimisha miaka 45 tangu kuanzishwa kwake, bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, DDC Mlimani Park (Sikinde ngoma ya Ukae) inatarajia kuanzisha ‘Academy’ kwa ajili ya kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wachanga ili waje kuwa warithi wazuri kwa maslahi mapana ya bendi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mratibu mkuu wa mipango na matukio ya bendi hiyo, Hassan Msumari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa DDC Keko jijini Dar es Salaam Septemba 5, 2023 kuhusiana na Wiki ya Sikinde ambayo imezinduliwa rasmi siku hiyo kuelekea kwenye shughuli kubwa ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwake.

“Bitchuka na baadhi ya wanamuziki wengine wa bendi yetu wanakwenda kustaafu, ili kuwapata warithi wao ili bendi iendelee tumekuja na wazo ambalo Tanzania halijawahi kuwepo, tunatarajia kuanzisha chuo cha muziki (Music Academy) kupitia mtaala ambao tutaupata kule Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) ambao utaletwa Sikinde baada ya kuonekana bendi yetu ni nembo ya nchi,” alisema Msumari.

Aidha mratibu huyo alisema kuwa shughuli yao, kutimiza miaka 45 ya DDC Mlimani Park itafanyika Septemba 30, 2023 siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, Dar es Salaam, kwa kiingilio cha shilingi 10 na kwamba sababu kubwa ya  kupeleka tamasha hilo hapo ni historia iliyonayo bendi yao na eneo hilo. “Bendi yetu iliasisiwa eneo la DDC Mlimani, Dar es Salaam ikawa na matukio DDC Kariakoo na hapo Magomeni Kondoa, kwa hiyo ni kiwanja cha nyumbani,” alisema Msumari.

vizazi vianze kurithishwa kazi hiyo baada ya kina Bitchuka na wengine kustaafu, yote hayo wakipata sapoti ya kutosha kupitia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo pia katika miaka 45 ya bendi yao itahusika kwa sehemu kubwa.

“Katika wiki ya Sikinde tutafanya mambo mbalimbali ya kijamii kuelekea kwenye tamasha hilo, ikiwemo kutembelea baadhi ya vituo vya watoto yatima, wagonjwa mahospitalini  na matukio mengine, tutatembelea vyombo vya habari (media tour) ili kuendeleza uhusiano wetu na Wana Habari,” alisema Msumari.

Bendi ya Sikinde ilianzishwa 1978, mpaka sasa imeshafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuhabarisha umma, kueneza na kuuthaminisha muziki wa dansi katika nchi yetu ya Tanzania, kupiga vita uzembe makazini, rushwa kupitia muziki, pia imefanikiwa kutoka nje ya nchi na kufanya matamasha katika baadhi ya nchi kama Ujerumani, Canada, Zimbambwe na kwingineko.

About The Author

(Visited 128 times, 1 visits today)

Last modified: September 6, 2023

Close