Visit Sponsor

Written by 3:05 pm KITAIFA Views: 99

MHE NDUMBARO ASISITIZA MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA MIKUTANO YA KIMATAIFA HAPA NCHINI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema  mikutano ya Kimataifa inayofanyika hapa nchini ni fursa ya kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili ambayo ni mojawapo ya Lugha Rasmi ya Kikazi ya Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya kadhaa za Kikanda Barani Afrika.  

Mhe. Ndumbaro amesema hayo  Oktoba 7, 2023  jijini Arusha katika kikao cha Maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu unaotarajiwa kufanyika  Oktoba 20 hadi  Novemba 9, 2023 jijini Arusha.

Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa, Tanzania ina  Wataalamu katika tafsiri  na ukalimani hivyo wana uwezo wa kutoa  huduma ya ukalimani katika Mikutano hiyo.

Kikao hicho kimeongozwa na Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana,Waziri wa Katiba na Sheria na kuhudhuriwa na Mhe.Haroun Suleimani,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

About The Author

(Visited 99 times, 1 visits today)

Last modified: October 7, 2023

Close