Igunga, Tabora Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa, anaanza ziara ya Kikazi Jimboni kwa ajili ya kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti kwa Wananchi, Kutatua kero za Wananchi na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Ngassa (MB) anaanza ziara ikiwa ni utaratibu wake wa kutoa mrejesho kwa Wananchi mara baada ya Bunge la Bajeti kukamilika.
Mheshimiwa Ngassa (MB) ataambatana wa Watalaam wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa ajili ya kutoa ufumbuzi wa kero za Wananchi.
About The Author
Last modified: July 5, 2023