Visit Sponsor

Written by 4:27 am KITAIFA Views: 4

MBUNGE BONNAH ACHARUKA ATAKA KUFUNGULIWA MARAMOJA NJIA ILIYOFUNGWA NA MFANYABISHARA WA KITUO CHA MAFUTA DAR

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli,  amesema yuko  tayari kutoa fedha zake  kugharamia uondoaji  mawe  makubwa  yaliyotumika na mfanyabiashara mmoja anayemiliki kituo cha mafuta kufunga  njia  na kusababisha  adha kubwa kwa wananchi kando ya daraja la juu linalovuka Reli ya  SGR,  Uwanja wa Ndege, Kata ya Kipawa, jijini Dar es Salaam.

Aidha  mfanyabiashara  huyo ametakiwa kujenga  sehemu aliyoboa ya daraja hilo  alipokuwa akiweka mawe hayo.

Bonnah ambaye leo alifika katika eneo hilo, amesema   mfanyabiashara huyo alipewa siku 14  aondoe mawe hayo na na kujenga sehemu  ya daraja aliyobomoa lakini hajatekeleza.

“Mimi nimeamua nitatoa fedha zangu, kesho Mwenyekiti wa CCM  Kata, Diwani na uongozi wa kata  wasimamie uondoaji wa mawe haya. Yasogezwe yawekwe pembeni wananchi watumie njia hii,”amesema Bonnah.

Wananchi wa eneo hilo, walimshukuru Mbunge huyo kwa uamuzi huyo kwani  hatua ya mfanyabiashara huyo kuziba njia katika eneo ambalo siyo mali yake  kiliwapa adha kubwa  kupia  kwenda katika nyumba zao  na kufanya shughuli zingine muhimu.



Katika hatua nyingine,  Bonnah ametembelea Soko la Buguruni  kusikiliza kero za wananchi  hususan sehemu ya kuchinjia kuku na kuahidi kuifanyia kazi.

Changamoto nyingine ni ya wafanyabiashara kuomba Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kurejesha choo cha umma katika soko hilo  katika uongozi wa soko badala ya kuendeshwa na halmashauri hiyo.

Bonnah aliahidi kuzitafutia ufumbuzi kero hizo haraka iwezekanavyo hivyo kuwataka wafanyabiashara kuendelea kutekeleza majukumu yao.

About The Author

(Visited 4 times, 1 visits today)

Last modified: December 5, 2024

Close