Visit Sponsor

Written by 3:37 pm KITAIFA Views: 22

MATUMIZI TEKNOLOJIA MBADALA YANAPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI WA BARABARA 50%

Matumizi ya Teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja imeweza kupunguza gharama zaidi ya 50%.

Hayo yameelezwa Jana na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Maelezo jijini Dodoma.

“TARURA imeweka kipaumbele cha kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.

Mhandisi Seff amesema  hadi kufikia mwezi Machi,2023 TARURA  imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua.

Ametaja mikoa iliyojengwa madaraja hayo ni Kigoma (92),Singida (24), Tabora (5), Kilimanjaro (10), Mbeya(2), Arusha (6), Morogoro (2), Rukwa(3), Pwani (1), Ruvuma (3) pamoja na Iringa (15).

Aidha, amesema bado wanaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.

“Teknolojia hizo ni pamoja na Ecoroads, Ecozyme na GeoPolymer ambao hadi Sasa kwa kutumia teknolojia ya Ecoroads katika jiji la Dodoma imejengwa Kilomita moja(1) ambayo imekamilika na katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa Kilomita kumi(10)”Aliongeza

About The Author

(Visited 22 times, 1 visits today)

Last modified: August 25, 2023

Close