Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi leo Aprili 8, 2024, ametembelea eneo la Jangwani ambalo Wakala ya Barabara Mjini na Vijijini (TARURA), inatarajia kuanza maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Bonde la Msimbazi ( Msimbazi Basin Development Project) utakaogharimu takribani shilingi Bilioni 660.
Katika Ziara hiyo Ameambatana na Mratibu wa Miradi inayotekelezwa kwa Ushirikiano na Benki ya Dunia TARURA Mhandisi Humphrey Kanyenye na viongozi wengine.


About The Author
Last modified: April 9, 2024