Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Mwandishi wa habari wa WazoHuru Media Ndg Mathias Canal amewata wananchi Mkoani Singida kuendelea kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibu ambaye ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba kutokana na kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika Taifa la Tanzania.
Amewataka wananchi kumuombea, kumtia moyo na kumpa ushirikiano ili aweze kufikia adhma yake ya kuwainua watanzania na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.
Mathias ameyasema hayo tarehe 2 Octoba 2024 wakati akizungumza kwenye mahafali ya 73 ya shule ya Msingi Kiomboi Hospitali iliyopo katika kata ya Old Kiomboi, Wilayani Iramba katika mkoa wa Singida.
Amesema kuwa Mbunge huyo anafanya kazi kubwa sio rahisi kuonekana jimboni mara kwa mara hivyo wananchi wanapaswa kumuombea na kumuunga mkono ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
“Sisi wanyiramba tuna bahati kubwa sana tuna Mbunge ambaye ni Waziri wa Fedha, Mchumi mbobezi ambaye amewahi kufanya kazi BOT, Lakini pia amehudumu nafasi mbalimbali ikiwemo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Katiba na Sheria. Vile vile alishawahi kuwa Mjumbe wa vijana wa UVCCM Wilaya ya Iramba, na Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa na sasa ni Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC)” Amesisitiza Mathias
Katika hatua nyingine Mathias amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuimarisha sekta ya elimu nchini hususani kuanzisha utaratibu wa wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba kuendelea na mafunzo ya miezi mitatu ya maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza jambo litakaloendelea kuwaweka pamoja wanafunzi na kuimarisha uelewa wao.
Katika mahafali hayo Mathias Canal amechangia jumla ya Shilingi 4,260,000 ikiwa ni kwa ajili ya madawati 36 yenye thamani ya Milioni 3,060,000, Motisha kwa Walimu 400,000, Vifaa vya Michezo jezi jozi nne na Mipira minne jumla 800,000, huku diwani wa kata ya Old Kiomboi Mhe Sadick Msengi akiwa amechangia madawati matano.
About The Author
Last modified: October 3, 2024