Na Sixmund Begashe
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nteghenjwa Osea amekabidhiwa rasmi ofisi na aliekuwa Mkuu wa Kitengo hicho Bw. John Mapepele ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, ili kuendelea kuwatumiaka wananchi kwenye ofisi yake hiyo.

Katika zoezi hilo la kihistoria lililofanyika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Patrick Marcelline alimpongeza Bw. Mapepe kwa Utumishi wake mwema kwenye Wizara hiyo na kumtakia kila laheri katika ofisi yake mpya, huku akimkaribisha Bi. Osea na kumuahidi ushirikiano wakutosha kwenye utekelezaji wa majukumu yake ndani ya Wizara hiyo inayojishughulisha na Uhifadhi pamoja na Utalii nchini.

Aidha Bi. Hossea ambaye awali alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini OR-TAMISEMI, ameushukuru uongozi wa Wizara hiyo kwa kumpokea vizuri na kuahidi Utumishi mwema katika kuiongoza vyema timu nzima ya mawasiliano ili kufikia lengo la Wizara na Taifa kwa ujumla kupitia Maliasili na Utalii, huku Bw. Mapepele akiushukuru uongozi, maafisa wa Kitengo cha Habari, Watumishi wote wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mzuri waliompatia katika kipindi chote alichohudumu hapo.
About The Author
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WIZARA YA TAMISEMI
Last modified: April 28, 2025