Visit Sponsor

Written by 10:43 am BIASHARA Views: 5

MAPENDEKEZO YA SHERIA WAFANYAKAZI WANAOJIFUNGUA WATOTO NJITI YAJADILIWA KAMATI YA BUNGE

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI


15 Januari 2025, DODOMA
————————————


Wadau mbalimbali wa masuala ya Kazi na Ajira kikiwemo Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE) ambacho ni moja ya Vyama vinavyounda Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA)  kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel Foundation ( DMF) leo Jumatano tarehe 15 Januari 2025 wameshiriki katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kilicholenga kutoa maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi wa Mwaka 2024 (The Labour Laws (Amendments) Bill, 2024 .

Katika kikao hicho, Wadau hao walioshiriki walipata nafasi ya kutoa maoni katika maeneo mbalimbali ya mswada huo kikiwemo kipengele cha nyongeza ya Siku za Likizo kwa Wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti ambapo wadau walipata nafasi ya kujadili kwa kina eneo hilo sambamba na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha na kuwa sheria kamili.


Akizungumza mara baada ya kuwasilisha mapendekezo yao, Katibu Mkuu wa TUGHE ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUCTA, Cde. Hery Mkunda ameushukuru Uongozi wa Bunge kwa kutoa nafasi kwa Vyama vya Wafanyakazi ambao ni wadau muhimu wa masuala ya kazi kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi wa Mwaka 2024 ambapo ameeleza kufurahishwa na namna ambavyo wadau wametoa maoni mazuri ya kuboresha vipengele mbalimbali vya sheria ikiwemo kwa wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti na kubainisha kuwa itakapokuwa sheria kamili itasaidia kutatua changamoto ambayo wafanyakazi hao wamekuwa wakikumbana nayo.



Kikao hicho kimehidhuriwa pia na Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Cde. Joel Kaminyoge sambamba wawakilishi kutoka Vyama vinavyounda Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: January 16, 2025

Close