Imebainika kwamba Watanzania wengi hasa wanyonge na masikini wamemizwa mioyo yao kwa dhuluma ambayo wamefanyikwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuporwa ardhi na watu wenye pesa ambao wana mitandao mikubwa ya kujuana na watu wanaoweza kuwalinda.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo Machi 5, 2024 katika ofisi ndogo za chama, Lumumba, Dar es Salaam kuhusu ziara ya mikoa 23 aliyoifanya kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya ilani na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Makonda amesema kuwa, katika ziara hiyo kikubwa walichobaini ni watu hasa wanyonge kudhulumiwa haki zao, ikiwemo kuporwa ardhi na wenye fedha, kupewa nyaraka au hati feki kitendo ambacho kama chama wameelekeza kila aliye na nafasi ana wajibu wa kutatua changamoto aliyopelekewa na mwananchi na afahamu ofisi aliyopo siyo yake ni ya umma na kutokutatua changamoto ya wananchi ni kuendelea kulimbikiza matatizo na kufanya wananchi waichukie serikali yao, au chama chao.
“Mioyo wa Watanzania wengi imeumizwa na dhuruma ambayo imegawanyika kwenye maeneo mengi, kilio cha watu kupewa nyaraka au hati feki kimetawala, katika eneo hili tulitoa maeleezo mahususi tarehe 19, wakati tunaanza ziara mkoa wa Dar es Salaam, Bunju. Myonge mnyongeni haki yake mpeni. Kama Idara ya Itidadi Uenezi na Mafunzo, tunatiwa moyo na jitihada zinazofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ndugu yetu Jery Silaa, tulimwelekeza aende katika mkutano tuliofanya sisi pale Bunju akakae na wananchi na aweke utamaduni wa kuhangaika na migogoro. Amekuwa akiifanya kazi hiyo usiku na mchana, ama kweli tunaona jitihada zake na utiifu wake kwa chama, rai yetu ni kwamba waendelee kufanya kazi hiyo,” alisema Makonda.
Aidha Mwenezi huyo wa CCM alisema kuwa, wale wote waliodhulumu na kunyang’anya haki za wananchi, wasisite, wawachukulie hatua hata kama zina maumivu, ziwe fundisho ili kumlinda mnyonge na masikini wa taifa hili asikandamizwe na watu wenye pesa na wenye mitandao mikubwa ya kujuana na watu wanaoweza kuwalinda.
“Sambamba na hilo tulikubaliana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hawa watu wote wanaotapeli ardhi za watu, hawafanyi peke yao, wanayo mitandao mikubwa inayowalinda, tunamsihi na kumuelekeza afanye mapitio ya watendaji wa Sekta au Wizara ya Ardhi, watakaobainika ni sehemu ya wana mitandao ya kudhurumu haki za watu hasa masikini bila kusita nao wachukuliwe hatua. Mtu amepewa hati juu ya hati, wanaotoa hati wako wapi, wamechukuliwa hatua gani?” alihoji Makonda.
Aliendelea kuwa wanachotamami kuona kama chama ni kwamba, kila mtu anafanya kazi yake pasipo kumuonea mtu mwingine, kweye ziara yake alipita na kuona, kazi inayofanywa na Waziri wa Ardhi inabidi iungwe mkono na wafanyakazi wote na wale ambao wamekuwa chanzo cha migogoro hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa utaratuibu wa kiutumishi.
“Kuhama tu siyo jawabu, tumeenda kwa mfano pale Iringa tumemkuta mtu mmoja almaarufu kama Shirima na wenzake wamekaa zaidi ya miaka 16, wengine wamekaa miaka 20. Mtendaji anapokaa kwa muda mrefu kiasi hicho, wakati taratibu za kiutumishi zinataka akae isizidi miaka 4, hao watu wanajenga mitandao. Hata tulipomsimamisha kwenye mkutano wetu kila mmoja alilia naye na kuonyeha jinsi gani hawawatendei haki”, alisema Mamonda.
About The Author
Last modified: March 5, 2024