Visit Sponsor

Written by 2:13 pm KITAIFA Views: 66

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA PAMOJA SJMT NA SMZ

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango ameongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya
kushughulikia Masuala ya Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden
Tulip Zanzibar tarehe 06 Machi 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia Masuala ya Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.

Makamu wa Rais amewapongeza viongozi na wataalamu wote walioshiriki katika kikao hicho kwa jitihada walizofanya wakati wa maandalizi na majadiliano. Amesema kikao hicho ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa na Muungano hivyo ni wajibu kuhakikisha lengo la kuulinda na kuutetea Muungano linafikiwa.

About The Author

(Visited 66 times, 1 visits today)

Last modified: March 6, 2024

Close