Visit Sponsor

Written by 1:27 pm KITAIFA Views: 5

MAKALLA AANZA ZIARA MKOA WA LINDI



*•Akagua barabara na madaraja  SOMANGA*

*•Atoa pole na kumshukuru Rais Samia kutoa fedha zaidi Bilioni 100 kujenga madaraja*

*•Ampongeza Waziri Abdallah Ulega na Tanroad kwa kuwahi na kusimamia matengenezo*

*KATIBU* wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi and Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewasili mkoani Lindi leo Aprili 10,2025 kwa ajili ya ziara yake katika mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.

Awali baada ya kuwasili mkuani humo alipita katika Kata ya Somanga Mtama iliyopo katika Jimbo la Kilwa Kaskazini mkoani Lindi kwa ajili ya kusalimia wananchi wa eneo hilo.

Aidha, Makalla kabla ya kusalimia wananchi hao alitembelea katika daraja la Somanga Mtama ambalo lilikatika na kupelekea kupotea kwa mawasiliano katika barabara ya Dar es salaam-Lindi na kuangalia hali inavyoendelea katika daraja hilo.

Akizungumza katika eneo baada ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kutoa ufafanuzi mfupi Makalla alimpongeza kwa weledi mkubwa aliouonyesha kwa kuweza kurudisha mawasiliano hayo kwa muda mfupi na kumtaka aendelee kuwa mkali pale uzembe unapotendeka kwani kile anachokifanya ni kwa maslahi ya CCM kwa sababu wana dhamana kwa wananchi.

Zaidi ya Sh bilioni 100 zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madaraja hayo, hivyo amemsisitiza Waziri Ulega kuhakikisha anasiamamia wakandarasi madaraja hayo yajengwe kwa ubora na kwa hadhi inauostahili kwani fedha zipo za kutosha.

CPA Makalla anatarajiwa kufanya mkutano wake hadhara na kuzungumza na wananchi katika eneo la Kilwa Masoko.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: April 10, 2025

Close