Visit Sponsor

Written by 1:37 pm KITAIFA โ€ข Views: 65

MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI SONGWE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa usambazaji umeme vijijini na vitongojini utakaogharimu sh. bilioni 5.2 na dola za Marekani milioni 10 ambao unatarajiwa kusambaza umeme katika vitongoji 171 vya wilaya za Mbozi, Ileje, Momba na Songwe.

Uzinduzi wa mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) umefanyika leo (Ijumaa, Novemba 24, 2023) katika kijiji cha Ivugula, kata ya Mahenje, wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Mkuu amesema uzunduzi huo ni kiashiria kuwa kazi ya kupeleka umeme vijijini inaendelea. โ€œHatua hii ni kutekeleza dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kila nyumba ya Mtanzania iwake umeme,โ€ alisema.

Akitoa taarifa ya Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili Mzunguko B (REDPIIB), Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti (REA), Mhandisi Godfrey Chibulunje alisema mradi huo unalenga kupeleka umeme katika vitongoji ambavyo havina umeme ila vimepitiwa na miundombinu ya msongo wa kati wa umeme.

Alisema Wakala wa Nishati Vijijini unatekeleza miradi mitano katika maeneo tofauti ya mkoa huo ambayo ni REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round II); na Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili B (REDPIIB). Mingine ni Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vitongoji (HEP); Mradi wa Kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na Mradi wa Kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji.

Alisema mkoa wa Songwe una vijiji 307 ambapo hadi sasa, vijiji 281 sawa na asilimia 91.5 vimepatiwa huduma ya umeme kupitia miradi mbalimbali ya umeme vijijini.

About The Author

(Visited 65 times, 1 visits today)

Last modified: November 24, 2023

Close