Visit Sponsor

Written by 7:43 am BURUDANI Views: 7

MAGESE JAJI MKUU SAMIA FASHION FESTIVAL

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

MWANAMITINDO  wa Kimataifa Mellen Happiness Magese ametangazwa kuwa Jaji Mkuu wa Tamasha la Samia Fashion Festival litakalofanyika leovisiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kutangazwa kuwa Jaji Mkuu wa Tamasha hilo , Millen Magese alisema kuwa ni heshima  kubwa.

Alisema kuwa ni furaha kwake kusimama kama Jaji Mkuu wa Samia wa Fashion Festival na kwamba anajivunia kushuhudia wakati huu wa kihistoria ambao unasherehekea ubunifu, stara, na urithi wa kipekee wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisema kwao wao walioteuliwa kuwa majaji “tunaamini kuwa tukio hili ni kubwa na litakalobakia katika kumbukumbu zetu kwa miaka mingi ijayo, kutokana na kuteuliwa kwetu kuwa majaji wa Samia Fashion Festival,”

“Kwa zaidi ya miaka ishirini, nimejitolea maisha yangu katika sekta ya mitindo, urembo, Nimezunguka duniani, nikifanya kazi na chapa kubwa na maarufu, nimeona  jinsi mitindo inavyothaminiwa katika nchi za Ulaya na mataifa mengine, si tu kama sanaa bali kama alama ya utambulisho, urithi, na fahari.

“Niliposikia kuhusu mpango huu wa kipekee, sikusita, nilichukua ndege haraka  kuja nyumbani kuwa sehemu ya safari hii ya kihistoria, kwa Tamasha hili si tu kuhusu mavazi; ni kuhusu heshima yetu kama Watanzania,”alisema.

Mwanamitindo huyo ambaye anaishi nchini Marekani kwa sasa alisema uandaaji wa Vazi la Samia alama ya stara, uongozi, na heshima ni zaidi ya mavazi ya kawaida. Ni kazi ya sanaa inayostahili kuhifadhiwa katika makumbusho kwa vizazi vijavyo, kama heshima kwa urithi wa kiongozi huyo.

Alieleza ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi kuona Vazi la Samia linakuwa ishara ya kitaifa na kimataifa, chanzo cha fahari kinachowakilisha uzuri, nguvu, na umoja wa Tanzania.

“Tukubaliane kufanya kitu cha kipekee, kitu kitakachotupeleka ulimwenguni na kuacha alama katika historia. Kwa wabunifu, wanamitindo, na wote wanaoshiriki, tambueni kuwa hampo tu katika sehemu ya tamasha, bali mnakuwa sehemu ya historia ya kizazi kitakachovutia dunia. Hebu tufanye wakati huu uwe wa kukumbukwa milele.”

Pia alisema  pamoja na yeye nami kuwa Jaji mkuu katika tamasha hilo anayofuraha , pia kuona jopo zima la majaji wenzake ambao watakuwa  pamoja katika shughuli hiyo adhimu na kusisitiza hoop hilo limesheni majaji wenye umahiri.

Pia ametoa rai kwa Watanzania kuendeleakuunga mkono juhudi za Rais Wetu Mama SamiaSuluhu Haasan ambaye tangu ameingia madarakani ameendelea kusimama imara kuhakikisha sektaya Utamadini katika tasnia ya Mitindo na Uremboinapewa nafasi kubwa katika nchi yetu.

Mbali na yeye wengine ni Idris Sultan ambaye ni Muigizaji na mchekeshajimashuhuri,Khadija Mwanamboka – ambaye ni Mbunifu maarufu namwanzilishi wa sanaa mbalimbali.Pia Jokate Mwegelo – ambaye ni Kiongozi mashuhuri naMalkia wa Urembo.

Wengine ni Martin Kadinda ambaye ni  Mbunifu maarufu wamavazi,Faraja Nyalandu  ambaye ni Kiongozi  wa Jami naMalkia wa Urembopamoja Nancy Sumari ambaye ni Kiongozi  wa Jami na Malkiawa Urembo.
Awali akizungumza kuhusu Samia Fashion Festival Mwanzilishi na Muandaaji wa Tamasha hilo Khadija Mwanamboka alisema amewashirikisha wanamitindo mbalimbali na kuungana nao katika tamasha hilo ili Kusaidia watoto wanaoishi na virusi Vya UKIMWI na Saratani.

Kwa upande Mwigizaji maarufu nchini İdris Sultan alisema anajisikia furaha kuwa sehemu ya walioshirikishwa katika eneo la majaji na kueleza umefika wakati kwa Watanzania kutoa nafasi kwa wanawake wenye uwezo ukiwemo uongozi na kusisitiza Rais Samia amekuwa mfano mzuri na wa kuigwa .

About The Author

(Visited 7 times, 1 visits today)

Last modified: December 3, 2024

Close