Visit Sponsor

Written by 4:17 pm KITAIFA Views: 81

MAANDALIZI MKUTANO HALMASHAURI, KAMATI KUU DAR ES SALAAM YAKAMILIKA- MAKONDA

Mkutano wa Halmashauri na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unatarajiwa kuanza Jumanne  Novemba 28, 2023 jijini Dar es Salaam kwa mafunzo kwa wajumbe na kuendelea Novemba 29, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za CCM, Lumumba Dar es Salaam  leo Jumatatu Novemba 27, 2023 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Christian Makonda  amesema maandalizi yote ya mkutano huo yamekamilika.

“Nachukua nafasi hii kuwakaribisha wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM  katika mkutano wake wa kawaida chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kikao ambacho kitaanza kwa mafunzo  ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu na kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu Novemba 29, 2023 hapa hapa Dar es Salaam”, alisema Makonda.

Aidha Makonda amesema kuwa anapenda kutumia fursa hiyo kuwataarifu wanachama, wapenzi  na wakereketwa kufuatilia kwa kina kikao hicho muhimu kitakachojadili mustakabali wa chama na hasa maendeleo ya Watanzania kwa ujumla.

“Nafahamu  mazingira ya Dar es Salaam ni mazuri na Wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ni wajumbe muhimu na kikao muhimu  na lengo la kutoa taarifa hii  ni kuwajulisha wanachama, wapenzi na wakereketwa wajue kwamba ratiba ya vikao katika ngazi ya juu ya Kitaifa  inaendelea  na ni sehemu ya kuongeza chachu ili kuanzia ngazi ya mashina, matawi kwenda kwenye kata, wilaya  wanapoona viongozi wao wanakutana kujadili mambo na mustakali mpana wa taifa lao katika uhai wa chama na wao wanapata morali ya kuendelea kuishi kwa mujibu wa  kanuni kwa kufanya vikao  kama ambayo kanuni zao zinaelekeza”, alisema.

About The Author

(Visited 81 times, 1 visits today)

Last modified: November 27, 2023

Close