Visit Sponsor

Written by 6:00 am BIASHARA Views: 11

“KODI HAINA HIARI,NI LAZIMA KWA KILA MTANZANIA”RC CHALAMILA

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ametoa wito kwa wadau wote kuungana  kuhakikisha kila mlipa kodi analipia kodi inayostahili
Ili kukuza uchumi wa nchi hususani Mkoa wa Dar es salaam.

RC Chalamila ameyasema haya leo Oktoba 2 ,2024 wakati akifungua Kongamano la Kodi lililofanyika ukumbi wa Julius Nyerere(JNICC) na   kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka TRA na OASIS FINANCIAL SERVICES.

RC Chalamila katika kongamano  hilo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juhudi zake kuhakikisha mapato yanaongezeka Nchini na kuelekezwa katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii kama vile Elimu, Afya, Maji, barabara na nyingine nyingi

Aidha RC Chalamila amepongeza taasisi ya OASIS kwa kuwa daraja Kati ya TRA na wafanyabiashara katika kutoa elimu ya kikodi ili kupunguza migogoro ya kikodi isiyo ya lazima

Sambamba na hilo RC Chalamila amesema kuwepo kwa mtindo wa “Control Number” imesaidia sana hivyo amependekeza wataalamu kuleta teknolojia nyingine iliyo pana zaidi  itakayoweza kusaidia katika upande wa ulipaji Kodi.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Oasis Group, Bwana Stambuli S. Myovela, alieleza kuwa kongamano hilo limelenga kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya kodi na kupata suluhisho endelevu, ambapo amesema  OASIS imejitolea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

Mwisho Mhe. Chalamila alihitimisha kwa kusema, “Kwa dhati kabisa naomba tuendelee kushirikiana na kupeana mawazo kubuni mikakati mipya ili kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kwa kiasi kikubwa katika makuzi ya kiuchumi.”

About The Author

(Visited 11 times, 1 visits today)

Last modified: October 3, 2024

Close