Visit Sponsor

Written by 1:16 pm KITAIFA Views: 7

KIKWETE: WATAFUTA KAZI NJE ZINGATIENI SHERIA, TARATIBU



NA MWANDISHI WETU- SAUDI ARABIA

SERIKALI imekemea Watanzania wanao kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa inasababisha kutojulikana walipo na shughuli wanazozifanya.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu ajira za Watanzania nchini Saudi Arabia uliyofanyika jana Januari 27. 2024 nchjni huko.

Waziri amesema uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Saudi Arabia hauruhusu wafanyakazi kufanya kazi au kusafiri bila kufuata utaratibu, hivyo kila Mtanzania anayehitaji kufanya kazi nje ya nchi apitie kwa mawakala wanatambulika baina ya nchi hizo mbili.

Kikwete amesema miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa Watanzania kusafiri kwenda nchini Saudi Arabia, upimaji wa afya, kupata kazi zenye staha na mshahara mzuri ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi.

About The Author

(Visited 7 times, 1 visits today)

Last modified: January 28, 2025

Close