Visit Sponsor

Written by 12:10 pm KITAIFA โ€ข Views: 24

KIKWETE AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTUMIA MIFUMO YA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na watumishi wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kupima utendaji kazi wa mtumishi na taasisi katika ukumbi uliopo Mkandarasi House Jijini Dodoma tarehe 19 Desemba, 2023. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais- UTUMISHI Bi. Felista Shuli.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Ofisi ya
Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Wakala wa
Huduma ya Ununuzi Serikalini-GPSA kuzingatia mafunzo wanayopewa
ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi na taasisi kwa jumla.
Mhe. Kikwete amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo
ya matumizi ya mifumo ya kupima utendaji kazi wa watumishi na taasisi
(PEPMIS, PIPMIS) na HR Assesment kwa nyakati tofauti.

Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kupima utendaji kazi wa mtumishi na taasisi katika ukumbi uliopo Mkandarasi House Jijini Dodoma.


Mhe. Kikwete ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inalenga kutoa
huduma bora zaidi kwa wananchi, hivyo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora imebuni mifumo hiyo kwa lengo la
kutatua changamoto za upimaji wa utendaji kazi wa watumishi na taasisi
na zaidi kutambua hali halisi ya uwiano wa rasilimaliwatu katika utumishi
wa umma.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema kuwa mfumo wa zamani wa upimaji
utendaji kazi wa watumishi kwa kujazaji fomu za OPRAS ulionekana
kushindwa kupima uhalisia wa kiutendaji kwa watumishi wa umma.
Hivyo mifumo hii ya PEPMIS na PIPMIS itatatua changamoto
iliyokuwapo hapo awali na kuleta ufanisi zaidi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji
Dkt. Tausi Kida ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kubuni na kusanifu mifumo
hii muhimu itakayoleta ufanisi wa kiutendaji na kuzingatia haki na wajibu
kwa watumishi wa umma na Serikali kwa jumla.
โ€œTumefurahia ujio wa mifumo hii ambayo italeta chachu kwa watumishi
wa umma katika kuwahudumia wananchi na kuifanya Serikali kuboresha
maeneo yenye changamoto kwa watumishi na taasisiโ€ Amesema Dkt.
Kida.
Dkt. Kida ameongeza kuwa ofisi yake iko tayari kuunganisha mifumo hii
ya PEPMIS, PIPMIS na HR Assessment kwenye Dira ya taifa ya mwaka
2050 ambayo itaenda kuonesha mwelekeo wa nchi kwa miaka 25 ijayo.

About The Author

(Visited 24 times, 1 visits today)

Last modified: December 22, 2023

Close