Visit Sponsor

Written by 5:19 pm BIASHARA, KITAIFA โ€ข Views: 13

KASI YA UPAKUAJI MASHEHENA BANDARINI YAONGEZEKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Kutokana na maboresho makubwa na matumizi ya vifaa na teknolojia ya kisasa, Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuvutia wafanyabiashara wengi kuitumia kwa usafirishaji wa shehena zao.

Akizungumza Katika ziara yake aliyoifanya Bandari ya Dar es Salaam,Tarehe 15 January 2025 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Bw. Hamis Livembe, amesema kuwa wameridhishwa na ufanisi mkubwa katika uhudumiaji wa shehena, ambapo huduma zinatolewa kwa muda mfupi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.


Livembe amesema kuwa wafanyabiashara wengi waliokuwa wameacha kutumia Bandari ya Dar es Salaam sasa wameanza kurejea baada ya kushuhudia maboresho makubwa katika utendaji, hali inayohakikisha shehena zao zinahudumiwa kwa haraka na kwa viwango vya juu vya ufanisi.

“maboresho yaliyofanyika bandarini hapo yameharakisha ufanyaji wa biashara nchini na hivyo kuongeza vipato vya wafanyabiashara na taifa kwa ujumla”Amesema Livembe



Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed, amesema kuwa muda wa kuhudumia meli za makasha umepungua kutoka siku 10 hadi 3, hatua inayoboresha mzunguko wa biashara na kuongeza ufanisi wa bandari. Aidha, matarajio ni kuhudumia jumla ya tani milioni 25 za shehena katika mwaka huu wa fedha unaoishia Julai 2025.

“Serikali kupitia bandari ya dar es salaamย  imewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuharakisha uchukuaji wa mizigo iliyopo bandarini kwani uwekezaji uliofanyika umeongeza ufanisi na kasi ya upakuaji wa shehena bandarini hapo”Amesema Gallus


Naye Elitunu Mallamia ambaye ni meneja mahusiano wa kampuni ya DP wolrd amesema kwa kipindi kwa mwezi disemba 2024 wamefanikiwa kuhudumia meli 16 na magari takribani 25251 hivyo wanaendelea kuboresha miundombinu ili kuongeza ufanisi zaidi

Maboresho haya yanaifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa kitovu bora cha biashara na lango kuu la usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

About The Author

(Visited 13 times, 1 visits today)

Last modified: January 15, 2025

Close