Visit Sponsor

Written by 11:10 am KITAIFA Views: 16

KAMANDA WA POLISI SONGWE ATOA POLE KWA MAMA ALIYEPOTEZA MUME NA MTOTO KWA MAUAJI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya ametoa Pole kwa mama aliyepoteza mume na mtoto wake kutokana na tukio la mauaji lililotokea Desemba 12, 2023 katika kijiji cha Hangomba Kata ya Bara wilayani Mbozi.

Kufuatia tukio hilo bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini waliohusika katika kutekeleza mauaji hayo na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Aidha, kamanda Mallya alitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Naye Martine Mbembela, Mwenyekiti wa kijiji hicho kwa niaba ya mama huyo aliyepoteza familia yake alilishukuru Jeshi la Polisi  kwa kuonesha ushirikiano na kufika kumpapole mama huyo kutokana na familia yake kukumbwa na mkasa huo.

About The Author

(Visited 16 times, 1 visits today)

Last modified: December 19, 2023

Close