Wanajumuiya kutoka kanda tano waliokaa na kutoa maamuzi ya kuwasimamisha wenzao wawili Jijini Mwanza
Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania imetoa tahadhari dhidi ya waliokuwa watumishi wake waliosimamishwa kazi kutokana na ukiukwaji wa maadili ili wasipokelewe na kuhusika na kazi za Jumuiya hiyo baada ya kuwepo tetesi kuwa watumishi hao wanaendelea kujihusisha na kazi za Jumuiya husika.
Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania imetoa tahadhari kwa Watanzania dhidi ya waliokuwa watumishi hao ambao ni Peter Sangija aliyekuwa Mkurugenzi wa idara ya vijana Taifa wa Jumuiya hiyo na Mchungaji Fredrick Mahanyu aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania ambao wawili hao hawapo tena katika nafasi zao tajwa huku Jumuiya hiyo ikiwataarifu Watanzania kuwaepuka watumishi hao kwa kutowapokea au kuwahusisha na masuala yahusuyo Jumuiya hiyo.
Watumishi hao wawili walisimamishwa nyadhifa zao kwa ukiukwaji wa maadili na makatazo yaliyowekwa ndani ya Katiba ya Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania baada ya kwenda kinyume na miongozo ya Jumuiya na kujivika madaraka ya Viongozi wao na kuleta sintofahamu baina ya Jumuiya, Serikali na jamii.
Kufuatia hali hiyo Jumuiya hiyo imetoa wito kwa Watanzania kutoendelea kuwasiliana na watumishi hao wala kutumiwa nyaraka yoyote kutoka kwao pasipokupata kibali maalum kutoka kwa Viongozi husika wa Jumuiya kuu huku ikielezwa kuwa atakayehusika au watakaojihusisha na waliokuwa watumishi hao watawajibika wenyewe kwa ngazi husika za Kiserikali.
Aidha Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania imeeleza kuwa kwa yeyote atakayehitaji msaada kutoka Jumuiya hiyo awasiliane na Viongozi pekee wanaohusika na Ofisi mbali mbali nje na ndani ya Jumuiya akiwemo Mchungaji Barnabas Michael Ngusa ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania, Mchungaji Deus Kayoka Makamu Mwenyekiti, Mchungaji Elias Kashambaghani ambaye ni katibu Mkuu, Nelson Penford Madamanya Naibu katibu Mkuu, pamoja na Silvanus Peter Cheyo Mweka hazina na wakili Magezi Jastus kuwa ndiye mtu pekee anayeweza kufanya mawasiliano na Ofisi mbali mbali ikiwemo kuwasilisha nyaraka au kupokea nyaraka kwa niaba ya Jumuiya hiyo.
Hata hivyo Jumuiya hiyo iliwasimamisha nyadhifa zao watumishi hao wawili mnamo Oktoba 10, 2023 kupitia maamuzi yaliyopitishwa na kikao cha kamati kuu ya Jumuiya kilichohusisha wajumbe kutoka Kanda tano ambazo ni Kanda ya Ziwa, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Pwani, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Nyanda za juu kusini kikao kilichofanyika katika Kanisa la Baptist Nyamanoro Jijini Mwanza lengo likiwa ni imani ya Jumuiya hiyo
About The Author
Last modified: December 30, 2023