Mawaziri wa Kundi la Nchi zilizoendelea kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi wameazimia kuwa na Msimamo wa Pamoja katika Masuala Muhimu yatakayojadiliwa katika Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano huo ulioanza Septemba 28 hadi 29, 2023 jijini Dakar, Senegal umehudhuriwa naWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Mhe. Dkt. Selemani Jafo.
Akizungumzia mkutano huo, Waziri Jafo amesemayaliyojadiliwa ni tathmini ya kidunia kuhusu utekelezaji wa Makubaliano ya Paris unaosisitiza haja ya kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuepuka kuongezeka kwa athari na kiwango cha ongezeko la wastani la joto duniani kuvuka nyuzijoto 1.5.
Pamoja na kiwango cha fedha za mabadiliko ya tabianchi kuongezeka imebainishwa bado ni kidogo na hakikidhi mahitaji hivyo, iliazimiwa kuwa matokeo ya tathmini hiyoyawe chachu ya upatikanaji wa fedha hizo.
Aidha, Dkt. Jafo amesema kuwa mkutanoulibainisha kuwa ahadi ya nchi zilizoendelea ya ukusanyanyaji wa Dola za Marekani Bilioni 100 ifikapo mwaka 2025 haijatimizwa, hivyo uhaba wa fedha ni changamoto kwa nchi zinazoendelea na hazikidhi mahitaji ya kukabiliana na changamoto zilizopo.
Kutokana na hali hiyoiliazimiwa kuwa taratibu za upatakanaji wa fedha kutoka katika Mifuko ya Mabadiliko ya Tabianchi zirahisishwe, kutimizwa kwa ahadi ya nchi zilizoendelea ya ukusanyaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi na umuhimu wa kuongeza kiwango cha fedha kukidhi mahitaji.
Dkt. Jafo amesema kuwa majadiliano hayo pia yalijikita kuhusu muundo wa Mfuko wa Kushughulikia Hasara na Uharibifu Utokanao na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi, taasisi itakayosimamia Mfuko, vyanzo vya fedha na utaratibu wa upatikanaji wa fedha kwa nchi zitakazokidhi vigezo.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa Mfuko huo haujaanza kufanya kazi hivyo, msisitizo ulitolewa uanze kufanya kazi haraka iwezekanavyo kutokana madhara na hasara kubwa za athari za mabadiliko ya tabianchi hasa kwa nchi zinazoendelea.
“Nchi zimeweka msisitizo kuwaMfuko upatiwe fedha haraka iwezekanayo kwa na hata nchi zote zinazoendelea kuwa na sifa na kustahili kutumia Mfuko huo na piakuwe na utaratibu rahisi wa upatikanaji wa fedha kutoka kwenye Mfuko, Fedha zinazotolewa ziwe msaada na si mkopo na pia kutoathiri kiwango cha fedha za kuhimili mabadiliko ya tabianchi,” amesema.
Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi(COP28) unatarajiwa kufanyika Novemba 30 hadi 12 Disemba, 2023 Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu (UAE).
About The Author
Last modified: September 29, 2023