Visit Sponsor

Written by 4:01 pm MICHEZO Views: 6

IBRA BACCA APANDISHWA CHEO KATIKA KIKOSI CHA KUZUIA MAGENDO (KMKM)

Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), kimempandisha cheo nyota wa timu ya Yanga SC, Ibrahim Hamad “Ibra Bacca” kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora kwenye mchezo wa soka.

“Sina budi kushukuru kikosi changu kwa kuweza kunisapoti kwa kila hatua. Nitaendelea kuipambania nchi yangu,” amesema Sajenti Ibrahim Bacca ambaye wazazi wake pia ni askari.

KMKM iliyomwachia Bacca kuitumikia Yanga, ni kikosi cha ulinzi cha Zanzibar ambacho kina jukumu la kulinda mipaka ya bahari dhidi ya magendo, uvuvi haramu, na vitendo vingine vya kihalifu. Pia, KMKM husaidia katika operesheni za uokoaji baharini na usalama wa majini.

Credit TBConline

About The Author

(Visited 6 times, 1 visits today)

Last modified: March 17, 2025

Close