
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Hospital ya Amana yapata Tuzo ya mshindi wa kwanza Katika utoaji huduma Bora Kwa jamii Kwa hospital zote 28 za rufaa za mikoa
Ameyasema hayo 11 April 2025 Katibu Tawala wa mkoa Dkt Toba Nguvila wakati akipokea Tuzo hiyo Katika hospital ya Amana Jana na kusema kuwa
Napongeza juhudi za Mhe Rais Samia Kwa kazi nzuri na Bora ambayo anayoifanya Katika Sekta ya afya Katika hospital zote za nchi ya Tanzania hasa Katika mkoa wa dar es salaam

“Mumeona wenyewe kwenye miundombinu Ambapo mganga mfawidhi Amesema vizuri sana kuwa miundombinu inajengwa na inaendelea kujengwa kila siku mumeona pia Katika vifaa Tiba, vifaa vingi vimekuja vya kisasa na vilivyokuwa Bora kabisa zamani vifaa kama sitiscani,Emoaraai,ilikuwa haiwezekani kwenye hospital Zaidi ya hospital ya TAIFA ya muhimbili lakini Leo hata amana tunavyo”.
Ameongeza kuwa”zamani mulikuwa na watumishi wachache sana lakini Leo hali imekuwa nzuri Zaidi Kwa maana mama yupo yupo kazini lakini mama hawezi kufanya kazi pekee lazima kuwe na wasaidizi Bora na msaidizi namba moja wa mama ni Mhe waziri wa afya Munavyoona.amana inasonga Kwa sababu inawatendaji wazuri”.

Nguvila Amefafanua kuwa Ni uchambuzi wa vigezo mbalimbali ambavyo vimewekwa na wizara ya afya Katika kupima ubora na utendaji wa hospital zetu wa TPI na imeonekana hospital ya Amana imefanya vizuri Zaidi Kwa ubora wa utoaji huduma kuliko maeneo mengine
Amesema malalamiko ya hospital hiyo yamepungua na hospital inamazingira nadhifu na safi na watumishi wote wapo nadhifu na wamependeza vifaa vipo Bora vifaa havijarundikana vipo Kwa mpangilio mzuri wataalumu Bora Class A

Nae Mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa Amana Dkt Bryceson kiwelu Amesema mafanikio haya ni matokeo ya timu na umoja ulipo Katika hospital ya rufaa ya Amana
Kupitia umoja Wetu na mshikamano wa miaka mingi kabla hata ya kufika hapa hospital ya Amana ilikuwa inafanya vizuri na Katika mashindano ya ngazi mbalimbali ikiwemo ambayo yanaratibiwa na timu yako ya afya ya mkoa Tulikuwa tunaongoza mfurulizo kuazia mwaka 2021,2022,2023 na mwaka Jana tulishindwa Kwa nafasi Moja Kwa maski Moja Katika ngazi ya mkoa hata ngazi ya kitaifa tulishika nafasi ya kwanza Katika kutoa huduma Bora hizo zilishindanishwa hospital za rufaa za mikoa peke yake na Tuzo hiyo ilitolewa na mkurugenzi wa Tiba wizara ya afya

Tumeendelea kuboresha maeneo yetu ya kutolea huduma na falsafa yetu ni “kumponya mtoa huduma Ili aweze kuponya wale ambao wanapata huduma”
Nao wananchi ambao wamekuja kupata huduma Katika hospital hiyo ya Amana waliweza kutoa maoni Yao

Farida Athuman mkazi wa ilala bungoni dar es salaam Amesema tunapata huduma nzuri tunapokelewa vizuri tunahudumiwa vizuri Katika vitengo ambavyo tunavyoenda tunashukuru na tunampa hongera Rais Wetu Kwa kutuboreshea majengo,na madaktari
Yusuph Panzi ni mkazi wa Tabata segerea Amesema tunahitaji wajitahidi Katika upande wa mapokezi na jinsi ya ulipaji.pesa Kuna changamoto sana “Kwa sababu unaweza ukaja na mgonjwa na amezidiwa sana Sasa kwenye malipo Kuna mzunguko mrefu wakijitahidi hapo na itaonekana hospital Bora Zaidi ya hapo walichokipata”.
About The Author
Last modified: April 12, 2025