Afika eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo baada tu ya kutua kutoka nchini Brazil
Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haitasita kubomoa majengo yote ya Kariakoo, iwapo tume iliyoundwa kuchunguza usalama huo takuja na mapendekezo hayo.
Sambamba na hilo Mkuu wa nchi amewataka watendaji wa Serikali kuwajibika kwa nafsi zao katika utoaji wa vibali vya ujenzi akitaka visimamiwe ipasavyo.
Rais Saia aliyasema hayo jaa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea katika jingo liliouawa watu Kariakoo, ambalo limesabisha vifo vya watu 20 hadi kufikia jana.
โTukio la kuanguka kwa jengo la ghorofa nne katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam limeigusa serikali na Watanzania kwa ujumla,โ alisema Rais Samia
Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa eneo hilo, Rais Samia alisema ni tukio la kutisha na linaacha kumbukumbu mbaya kwa manusura wa janga hilo na Watanzania kwa ujumla.
Alisema kuanguka kwa jengo hilo kunaingia kwenye historia ya majanga ya kutisha yaliyowahi kuikumba nchi yetu.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa mpaka kufikia hii jana Watanzania 20 wamepoteza maisha kufuatia ajali ya kuanguka kwa jengo la ghorofa nne katika eneo la Kariakoo mkoani Dar es Salaam
Rais Samia alisema pamoja na vifo hivyo, majeruhi waliopo hospitalini ni watatu pekee.
Alisema, ameuona umoja wa Watanzania katika tukio hilo na kwamba kila mmoja ameonesha moyo wa kuokoa wengine na sio kuchukua mali zilizopo kwenye jengo hilo.
About The Author
Last modified: November 21, 2024