Visit Sponsor

Written by 1:32 pm KITAIFA Views: 54

HABARI PICHA: SERIKALI YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA UKOMO WA BAJETI 2024/2025

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha na Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.39. Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza wakati akifunga rasmi hafla fupi ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwenye Kamati ya Bunge zima, katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.38.

Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.38.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) (kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, wakizungumza baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44,38.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Bw. Benjamin Chilumba, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.38.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akipongezana na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) (Kushoto), baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.38. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Akida.

About The Author

(Visited 54 times, 1 visits today)

Last modified: March 11, 2024

Close