Kampuni ya kizalendo, Fanikiwa Microfinance inayojishughulisha na utoaji mikopo nchini imewanufaisha Watanzania wengi ambao walitimiza vigezo na kufanikiwa kupata mkopo huo wakajikwamua kimaisha kwa kipindi kifupi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana kiongozi mkuu wa taasisi hiyo, Furaha Mabeyo alisema kwamba kupitia taasisi yao wameweza kuwainua watu wengi waliokuwa na uhitaji wa mikopo na kuwapatia kwa dhamana ya kadi ya gari.
“Kampuni yetu ipo kwa ajili ya kuendeleza mtu anayeenda kufanya biashara, siyo kumpa mtu aende akaanzishe biashara, hata kama anakuja kwetu kuchukua mkopo anaenda kuanzisha biashara lazima awe na kipato kitakachomuwezesha kufanya rejesho letu,” alisema Furaha.
Aidha kiongozi huyo aliyeambatana na watendaji wa ofisini yake alisema kuwa mpaka sasa taasisi yao ina wateja zaidi ya 2000, lengo ni kuongeza wengine wengi zaidi ndiyo sababu iliyowasukuma kuja kwenye vyombo vya habari kwa ajili ya kuuhabarisha umma wa Watanzania kuhusu huduma zao.
“Tunatamani watakuwa wengi zaidi kwakuwa huduma yeti ni nzuri, ndio maana tumefungua matawi sehemu mbalimbali nchini. Tulianza Dar es Salaam ofisi yetu mama ikiwa maneneo ya Moroco, tukaenda Moshi, Dodoma na sasa hivi tumefungua branch yetu nyingine hapa Mwenge kwasababu ya uhitaji wa watu wengi”, alisema Furaha.
Vilevile aliendelea kuwa hivi sasa wana mpango wa kuendelea kufungua matawi sehemu nyingine nchini wakianzia na Mbeya, Arusha,Tanga, Morogoro na kwingine kwakuwa wanatamani huduma yao iwafikie watu wengi nchini. Pia mbali na kutoa mikopo kwa dhamana ya kadi ya gari, wamekuwa wakiwawezesha hata wale wafanyabiashara wadogo wenye mitaji ya hadi laki moja.
“Wito wangu kwa wateja wetu waje kwa wakati, wasiogope ili mradi tu awe Mtanzania ambaye anajishughulisha na anaweza kufanya rejesho anakaribishwa, kama wewe ni mteja wetu mzuri amabaye ulikopa ukalipa kwa wakati, ukija mara ya pili hata kama gari lako lina thamani ya milioni tano, tunaweza kukukopesha hata milioni 10. Kwa wale ambao watapenda kuwa wateja wetu baada ya kusikia ujumbe huu wanaweza kuwasiliana name moja kwa moja kuitia simu no 0716 537923. Fanikiwa tupo kwa ajili yenu, tunatamani tufanikishe ndoto ya kila Mtanzania,” alisema Furaha.
About The Author
Last modified: October 3, 2023