Visit Sponsor

Written by 7:48 am KITAIFA Views: 5

DKT SAMIA AMLILIA NDUGULILE,ATUMA SALAMU ZA POLE



Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

OFISI ya Bunge imefanyia mabadiliko ratiba ya maziko ya Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Kanda ya Afrika, ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile ambaye amefariki usiku wa kuamkia Novemba 27, mwaka huu nchini India,  ambapo ratiba ya sasa inaonesha atazikwa Jumamne Desemba 3, 2024 Kigamboni Jijini Dar es Salaam badala ya Jumatatu.

Mwili wa Ndugulile utawasili leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukitokea nchini India na Jumatatu Desemba 02, mwaka huu utaagwa viwanja vya Karimjee kisha Desemba 3, 2024 wananchi wa Kigamboni watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho katika Viwanja vya Machava na baadaye atazikwa saa 9:30 Alasiri Kigamboni.

Awali taarifa za kifo cha Dkt. Ndugulile kilitangazwa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

Kabla ya kifo chake, Ndugulile alihudumu kama mbunge wa Kigamboni mkoani  Dar es Salaam, ambapo pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya kati ya mwaka wa 2017 na 2020 na Waziri wa Habari, Mawaasiliano na Teknolojia ya Habari hadi mwaka wa 2021.

Alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika Agosti mwaka huu na alitarajiwa kuanza majukumu yake Februari mwakani, akimrithi Dkt. Matshidiso Moeti aliyehudumu katika wadhifa huo kwa mihula miwili.

Katika hotuba yake ya kuukubali wadhifa huo, Ndugulile alielezea dhamira thabiti ya kuendeleza sekta ya afya na ustawi wa watu barani Afrika.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi akielezea kifo chake kuwa msiba mkubwa, naye Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus akisema ameshtushwa na kuhuzunishwa na kifo chake.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alisema mipango ya kuurejesha mwili wake nyumbani inaendelea.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: December 3, 2024

Close