Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Ni uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 Jijini Arusha, aamuru kurejeshewa kwa Ardhi yao na milioni 500/- mali za kanisa hilo
-ARUSHA
HATIMAYE mgogoro umehimisha. Ndivyo unavyoweza kuwa hasa baada ya hatua ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuelekeza kurejeshwa kwa eneo la takribani mita za mraba 7503.
Pamoja na hali hiyo pia Mkuu huyo wan chi ameagiza kiasi cha Shilingi milioni 500 zilizokuwa mali ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto wa Yesu nazo zikabidhiwe kwa kanisa hilo Jijini Arusha.
Akitangaza uamuzi huo jana kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, alisea kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 kati ya kanisa hilo na Serikali kumfikia Waziri wa Nchi, Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa Serikali ililichukua eneo hilo kwa matumizi yake na kisha baadae kulitaka Kanisa hilo kutoa Shilingi milioni 500 za kulipia eneo hilo wakati kanisa lilipoanza mpango wake wa kuongeza eneo la utoaji wa huduma mbalimbali kanisani hapo.
“Kwa niaba ya Rais leo kwa furaha kubwa ninapenda kutoa maelekezo ya Mheshiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameagiza eneo la Ardhi la kanisa lilirudi pamoja na kisi cha Shilingi 500. Hivyo ninaamini hatua hii sasa kanisa litakuwa huru kundeleza eneo lake,” alisema Makonda
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Mhashamu Baba Askofu Dkt. Isaac Amani, alimshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwa mtatuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi huku akikemea ubinfasi, ubabe na kutojali maendeleo ya wengine pamoja na ulafi kwa baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu nchini.
About The Author
Last modified: October 21, 2024