Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan amemteua Mhandisi Dkt. Prosper Lutangilo Mgaya kuwa Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Dkt. Mgaya anachukua nafasi ya Prof. Zacharia Mganilwa ambaye
amemamliza muda wake.
Uteuzi huu umeanza tarehe 04 Machi, 2024.
About The Author
Last modified: March 6, 2024