Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), akieleza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wakati alipoongoza ujumbe wa Wizara yake walipokutana na ujumbe wa Wizara ya Fedha ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa ajili ya kujaili maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) (wa kwanza kushoto), wakiwa na kikao kilichowashirikisha wajumbe kutoka pande hizo mbili kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour na wajumbe wengine wakiteta jambo, baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Mawaziri hao uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya ujenzi ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake katika Uchumi na maendeleo ya watu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – maamry Mwamba (wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Mhandisi Aisha Amour, wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Mawaziri hao ulioangazia maendeleo ya Wizara ya Ujenzi, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
About The Author
Last modified: March 19, 2024