Visit Sponsor

Written by 12:33 pm KITAIFA Views: 25

DKT NCHEMBA AKUTANA NA EXIM BANK CHINA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, akiongoza Ujumbe wa Tanzania mjini Beijing China, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Exim Mhe. Ren Shengjun na Makamu wake Mhe. Zhang Wencai, ambapo masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki hiyo na Tanzania yalijadiliwa kwa kina. Ikumbukwe kwamba Exim Bank wanafadhii miradi mbalimbali nchini Tanzania ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR.
Ziara ya Ujumbe wa Tanzania nchini China katika Taasisi Benki hiyo, imewashirikisha pia Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki na viongozi wengine kadhaa waandamizi wa Serikali

About The Author

(Visited 25 times, 1 visits today)

Last modified: August 21, 2023

Close