Visit Sponsor

Written by 1:46 pm KITAIFA Views: 39

DKT. MSONDE ASISITIZA WALIMU KUPEWA HUDUMA BORA

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akikagua moja ya miundombinu ya elimu inayojengwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Uyui akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Elimu na Maafisa Utumishi
pamoja na watendaji wengine kuwahudumia vizuri walimu pindi
wanapowasilisha changamoto zao ili zifanyiwe kazi.
Dkt. Msonde amesisitiza utoaji wa huduma bora kwa walimu nchini, wakati
wa vikao kazi vyake na Menejimenti za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui,
Igunga na Nzega Mji ambavyo vililenga kuhimiza uwajibikaji na kufanya
tathmini ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya
elimu katika Halmashauri hizo.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akihimiza uwajibikaji kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Nzega katika kikao kazi chake cha kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu kwenye Halmashauri hiyo.


Dkt. Msonde amesema, walimu wanalalamika kujibiwa vibaya pindi
wanapowasilisha changamoto zao kwa watendaji, na kuongeza kuwa
Maafisa Elimu na Maafisa Utumishi ndio wanaolalamikiwa sana kwa kutoa
kauli mbaya dhidi ya walimu ambao ndio wamepewa jukumu kubwa la
kulea watoto na kuwapatia ujuzi.
“Walimu wanalalamika na kuwasilisha ushaidi wa sauti zilizorekodiwa za
maafisa wote waliowajibu vibaya, ukisikiliza namna Afisa Utumishi au Afisa
Elimu alivyomjibu mwalimu inaumiza sana na unaweze kutokwa na
machozi hivyo wanapaswa kubadilika,” Dkt. Msonde amesisitiza.

Baadhi ya watendaji wanaounda Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Nzega wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde wakati wa kikao kazi chake cha kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu kwenye Halmashauri hiyo.


Dkt. Msonde amesema, maafisa hao wanapaswa kufahamu kuwa Mtumishi
wa Umma anapaswa kutoa huduma nzuri kwa watumishi wengine na
wananchi wanaofuata huduma katika maeneo yao ya kazi.
Ameongeza kuwa, mwalimu au mtumishi yeyote akiwasilisha hoja hata
kama haina mashiko asijibiwe vibaya, akitoa mfano wake mwenyewe na
wa Mhe. Waziri kuwa wanapokea malalamiko ya walimu 200 hadi 300 kwa
siku lakini hawatoi kauli mbaya kwa walimu hao.

About The Author

(Visited 39 times, 1 visits today)

Last modified: June 28, 2023

Close