Visit Sponsor

Written by 12:26 pm KITAIFA Views: 32

DKT. MPANGO AREJEA, AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA VEMA MITANDAO YA KIJAMII

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri

Maria Theresa Ledochowska, Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo tarehe 10 Desemba 2023 ambayo iliongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaasa watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii, kwani matumizi yasiofaa kwenye mitandao hiyo yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mungu.

Aidha Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.

About The Author

(Visited 32 times, 1 visits today)

Last modified: December 10, 2023

Close