Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza vitendanishi chenye jina la Action Medeor International Health Care katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo Kibaha mkoani Pwani jana Septemba 22, 2023.
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2023/09/Mollel-2-1024x683.jpg)
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Dkt. Mollel alisema Waziri Mkuu alipenda awepo kwenye shughuli hiyo lakini kwasababu ya majukumu mengine amemtuma yeye, ila amemuomba awaambie wote waliohudhuria hafla hiyo kuwa wakiona Rais Samia anatembea sehemu mbalimbali duniani ni kukutana na wenzao wenye teknolojia mbalimbali kasha kuwaunganisha na kuwaleta Tanzania ili wazalishe tunachokiitaji, ikiwemo kutengeneza ajira na mengine.
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2023/09/IMGM7959-1024x514.jpg)
“Leo tumeona mfano mzuri wa PPP, tuna Wachina, Wajerumani na watu wengine wameungana na kuja na hiki kiwanda, asanteni sana Watanzania ambao mmeweza kukidhi mahitaji yao na wananiambia mna vijana wazuri sana. Humu ndani ya Tanzania kuna vichwa vizuri sana, ntamwambia Waziri Mkuu akamwambie Mhe. Rais kwenye kile kiwanda kuna vijana wazuri wenye akili sana, asanteni sana”, alisema Dkt. Mollel
Aidha Dkt. Molle amewaomba Watanzania wanaoshirikiana na wawekezaji hao katika kiwandani hicho cha kuzalisha bidhaa za afya wajiongeze ili kupata maarifa zaidi, wasiwe ni watu wa kujifunza ABC namna ya kuendesha tu mashine au namna ya kuhakikisha wanachotaka kitokee, “Lakini tujiongeze na sisi kama wale vijana ambao wamekweda wakaangalia mashine ya moyo, wakafikiria jinsi ya kutengeneza cha kwao pembeni”.
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2023/09/kIWANDA-1024x683.jpg)
“Ninategemea nyie ifiki mahali hata tukisema tunaanzisha kutengeneza reagent wenyewe na kuproduce muwe na uwezo huo, mmejifunza kwa hawa. Nimeshawaomba hawa wapendwa, tuna watu wetu na tumenunua teknojia nyingi, leo ukisikia trioni 6 zimenunua mashine nyingi sana, hapa kuna dada ameniambia yeye anawajengea wenzie uwezo wa kutumia mashine, sasa angalia hospitali yetu ya mkoa inamlipia malazi, inamlipa DM, anaenda analala vizuri wiki mbili na anarudi na pesa ya kutosha, lakini afundishe watu wetu pale.
Dkt. Molle alimaliza kwa kuwaomba Watanzania kuwapa ushirikiano wawekezaji hao na kwamba yeye atakuwa balozi wao, ikiwezekana kuongeza viwanda vingine kama hivyo. Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Kiwanda hicho, Christoph Bonsmann alisema kuwa tayari wametoa ajira zaidi ya 20 kwa Watanzania na kwamba siku zinavyoendelea wataajiri zaidi huku wakizingatia taratibu za kulipa kodi kulingana na sheria za nchi, pia wataendelea kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazokidhi viwango na ubora ili kuwasaidia Watanzania katika masuala ya huduma ya upatikanaji wa matibabu
About The Author
Last modified: September 23, 2023