Visit Sponsor

Written by 2:31 pm KITAIFA Views: 7

DKT HUSSEIN  ALLY MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA KIBADA, MWASONGA – KIMBIJI

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

-Ikiwa ni Shamra Shamra kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kibada mwasonga hadi kimbiji yenye kilometa 41 na kuagiza ikamilike kwa wakati na kwa viwango huku akisisitiza suala la amani ya Nchi kwani ndio msingi wa kuimarika kwa miradi yote

Akizungumza leo April 25,2025 Wilaya Kigamboni Jijini Dar es salaam katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kibada-Mwasonga hadi kimbiji kwa kiwango cha lami Rais Dkt Hussen Mwinyi amesema uwepo wa amani ndio jambo lililowezesha ujenzi wa barabara hiyo ya kibada na zingine nyingi hivyo ni muhimu kuendelea kudumisha amani ambapo ameagiza ikamilike kwa wakati na kwa ubora.

Akizungumzia suala la muungano Dkt Mwinyi amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kudumisha muungano na kuendelea kumaliza kero za muungano jambo ambalo limezidi kuimarisha umoja

Awali kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar kuongea akiongea kwa niaba ya waziri wa ujenzi Waziri wa Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Jerry Silaa amesema barabara hiyo imekuwa ni kilio cha muda mrefu cha wananchi na sasa kwa ujenzi huo inakwenda kuifungua kigambani kiuchumi kwa kuwezesha wawekezaji kufanya kazi kwa ufanisi

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amemhakikishia Rais wa Zanzibar kuwa Mkoa upo salama na utaendelea kuwa salama licha ya uwepo vuguvugu la kisiasa huku akimppngeza Rais Dkt Samia kwa kuwezesha barabara hiyo kujengwa pamoja na kuwezesha miradi muhimu ikiwemo ya umeme sanjari na kumpongeza Rais Mwinyi kwa kuboresha miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar

Aidha Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo yenye jumla ya kilometa 41 Mtendaji mkuu wa TANROAD Mhandisi Muhammed Besta amesema ujenzi wa barabara hiyo umegawanywa kwenye vipande viwili ukigharimu kiasi cha shilingi bilioni 83.8 chini ya mkandarasi wa kampuni ya Estim na tayari ujenzi hadi sasa umefikia asilimia 30

Mwisho uzinduzi huo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya kaulimbiu isemayo ”Muungano wetu,heshima na tunu ya Taifa’ shiriki uchaguzi mkuu wa mqaka 2025″

About The Author

(Visited 7 times, 7 visits today)

Last modified: April 25, 2025

Close