Visit Sponsor

Written by 4:22 pm KITAIFA Views: 76

CHONGOLO AIPONGEZA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI DODOMA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameipongeza serikali katika kutatua changamoto ya maji jijini Dodoma
Chongolo ameyasema hayo wakati alipokwenda kukagua mradi wa maji ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Dodoma.
Alisema serikali imefanya kazi kubwa katika kuelekea kutatua changamoto ya uhaba wa maji kwa kutekeleza miradi ya maji.
“Kazi kubwa kubwa inayofanywa katika kutekeleza miradi ya maji kunatafsiri kuwa mnaelekea kutatua changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi na kuimarisha uhai wa wananchi, kwa hayo ni muhimu kwa kweli niipongeze sana serikali.”
Naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde aliiomaba serikali kuharakisha ulipaji fidia kwa wananchi ambao wameridhia kupitisha mradi wa maji Nzuguni.
Pia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia uchimbaji wa visima pembezoni ikiwemo mradi wa Nzuguni.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Aron Joseph alisema kutokana na ongezeko la watu, uhaba wa maji ni asilimi 50 ya majitaji katika jiji la Dodoma hatua ambayo imefanya mamlaka kwa kushirikiana na wizara kuendelea kutafuta vyanzo mbadala vya maji. Alitaja baadhi ya miradi ya muda mfupi kuwa ni uchimbaji wa visima vitano vyenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 7.6 kwa siku, ambayo yataongeza uzalishaji kutoka lita milioni 68.6 ya sasa hadi lita 76.2 kwa siku sawa na ongezeko la asilimia 11.7

About The Author

(Visited 76 times, 1 visits today)

Last modified: June 26, 2023

Close