Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Chama cha wananchi-CUF kimetoa wito kwa wafanyabiashara wa bidhaa za chakula kutokupandisha bei ya bidhaa hizo ili wapate faida mara dufu wakati huu ambapo waumini wa dini ya kiislalm wakiwa katika mfungo wa Mwezi mtukukufu wa Ramadhan.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho,Taifa Prof Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam Leo jumapili March 2,2025 juu ya masuala mbalimbali.
Lipumba amesema kwa wakati huu ni vyema wafanyabiashara hao kuuza bidhaa za chakula kwa bei ambayo huwa wanauza ili waendeleze kupata thawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu na si kuwakomoa wengine kwa kutaka faida kubwa.
Aidha Chama hicho pia kimewatakia waumini wote wa dini ya kiislam hapa nchini mfungo mwema wa mwezi mtukukufu wa Ramadhan
About The Author
Last modified: March 2, 2025